Habari za leo ndugu msomaji unayefuatilia blog hii ya Mchumi Faraja Mmasa,natumaini ni mzima wa afya njema.Leo nimependa kuongelea swala la namna ya kumfundisha mtoto nidhamu ambalo naona limekuwa tatizo katika familia nyingi hasa hapa Tanzania,wazazi wamekuwa wanapenda watoto wao kuwa na tabia njema lakini mwishoni wamepata matokeo wasiyoyategemea.
Nidhamukwa mtoto ni kumfundisha mtoto jinsi ya kujitawala
katika njia sahihi.Kumfundisha mambo anayotakiwa kufanya na asiyotakiwa
kufanya,pia kumsahihisha na tabia ambazo sio sahihi, pia kumfundisha nidhamu
huambatana na kumpongeza ,kumlinda, na kuonyesha ni namna gani unampenda.Kumfundisha
mtoto sio KUPIGA TU,wazazi
wengi hasa Waafrika tumekuwa na mawazo ambayo siyo sahihi kuhusu kumfundisha
mtoto nidhamu,wengi tunafikiri kumfundisha mtoto nidhamu ni KUCHAPA NA KUWA
MKALI MUDA WOTE.Kujua kumfundisha mtoto nidhamu kwa njia sahihi na
zinazokubalika ndio huleta tofauti kati ya mtoto mwenye tabia njema au nzuri na
Yule mwenye tabia mbaya au nidhamu mbaya.Mara nyingi wazazi huwa tunatumia njia
ambazo huwa sio sahihi kumfundisha mtoto nidhamu matokeo yake huwa tunapata
matokeo mabaya kwa watoto wetu,unakuta
wazazi wakali sana lakini mtoto kaharibikiwa hii inatokana na kutokujua mbinu
na njia sahihi ya kumfundisha mtoto nidhamu,leo ninataka kuongelea kwa undani
namna ya kuwafundisha watoto nidhamu na kupata matokeo mazuri kwa maana ya
watoto wetu kuwa natabia njema inayokubalika katika jamii yoyote
inayomzunguka.Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kuwafundisha watoto wetu nidhamu
nzuri au tabia njema;
1. KUWA NA MSIMAMO WA MOJA
KWA MOJA SIKU ZOTE
Kumfundisha mtoto nidhamu nzuri unatakiwa kujua kuwa
kuwa na msimamo pasipo kubadilka ndio jambo la msingi katika kumfanya mtoto
anakuwa natabia nzuri.Wazazi kuwa na msimamo mmoja ya kwamba tabia fulani ni
mbaya hata siku moja haikubaliki kwani huleta matokeo mabaya na tabia fulani ni
nzuri na ndio zinakubalika,mtoto anatikiwa kufahamu msimamo wa wazazi wake siku
zote za maisha yake kwamba jambo Fulani halikubaliki,wazazi mnatakiwa kuwa na
msimamo sio leo kafanya tabia mbaya hamchukui hatua kesho akifanya tabia ile
ile mnamgombeza au kumuuonya
2. TABIA YA WAZAZI IWE
MFANO HALISI
Hili ni jambo la msingi katika malezi ya mtoto
hakikisheni tabia zenu wazazi ndio kielelezo kwa mtoto,mtoto aige tabia njema
kutoka kwenu,sio mnawafundisha watoto tabia nyiyi wazazi ambazo mnazifanya
kinyume chake.Ni rahisi sana mtoto kuwa natabia njema kama mzazi wake anatabia
zinazostahili katika jamii,mzazi hakikisha unachohaidi kwa watoto unatimiza ili
watoto wajifunze tabia ya uaminifu na ukweli kutoka kwa mzazi.
3. WAZAZI KUTUMIA NJIA
MOJA ZA UFUNDISHAJI
Hili ni jambo la msingi zaidi katika malezi ya mtoto
kumfanya kuwa na tabia njema au nzuri,wazazi hakikisheni mnazungumza na kupanga
njia sahihi za kutumia kuwafunza watoto wenu,mara nyingi unakuta wazazi
wanatofautiana njia anazotumia baba ni tofauti na mama,hii mnachangaya watoto
na wakati mwingie mama anaweza kumwonya mtoto lakini mtoto kajibu mbona baba
alisema hivi? Au watoto huweza kupunguza mapenzi kwa mzazi mmoja kwa kuona anawaonea tofauti na mwingine ndio maana wakati
mwingine watoto husikia wakisema bora mama kuliko baba
4. KUKUBALI MABADILIKO
WAKATI MWINGINE
Mtoto ni mtoto,tegemea mabadiliko kwa mwanao wakati
mwingine,mtoto hawezi kuwa sahihi muda mwingine hata kama upo makini sana katika
kufuatilia nidhamu ya mwanao,pia mtoto muda mwingine hushikwa na hasira,kwa kwa
hiyo unahitaji umakini katika hili.
5. MUELEZE SABABU YA
KUMKATAZA KUFANYA KITU FULANI
Ni vizuri unapomkataza mtoto kumfanya kitu Fulani,kama
mtoto bado mdogo labda miaka miwili ni vizuri kumwambia kwanini unamkataza ili
hata atakapokuwa peke yake asifanye ,kwa mfano “usichezee huo wembe” mpe
sababu kwamba utamkata na kumpa kidonda halafu utamuumiza ,kwa hiyo siku nyingine
hata akiwa peke yake hatachezea.
6. USIMGOMBEZE KILA WAKATI(USIWE MTU WA KUFOKA FOKA BILA SABABU)
Mzazi ni muhimu kuwa makini katika swala la kumuonya
mtoto,usiwe mtu wa kugombagomba kila wakati ,hii itasababisha watoto kuzoea
hali hio na wawe waigizaji wa tabia,tumia muda mwingi kuwaeleza kwa upendo kwa
nini unawakataza ,kuwa mkali pale inapobidi na sio wakati wote.mwishoni itajijenga
vichwani mwa watoto mzazi wao ni mtu wa makelele na wasionyeke tena,ndio maana
unaweza kukuta baba na mama wakali sana lakini watoto wao hawana nidhamu pale
wazazi wao wanapokuwa hawapo karibu yao na ukubwani huharibikiwa kabisa.
7. MPONGEZE IKIBIDI MPE
MTOTO ZAWADI ANAPOFANYA VIZURI
Mzazi uwe na kawaida ya ya kumpongeza mtoto kila wakati anapofanya
kitu kizuri,hii itamfanya mtoto kujitahidi mara kwa mara mtoto kufanya kitu kizuri maana anajua anamfurahisha mzazi
wake na pale akifanya jambo zuri kabisa mpe zawadi ,hii itamfanya mtoto
kujiamini zaidi kufanya mambo mazuri,mzazi usiwe mtu wa kusema mabaya tu ,we
kazi yako kusema mabaya tu mazuri yote unakaa kimya,kila siku ukikuta nyumba
safi husemi lakini ukikuta siku moja tu ipo chafu ndio maneno yatakutoka mpaka
povu mdomoni na maneno machofu utatoa.
8. HAKIKISHA UNAMUONYESHA
MTOTO WAKO UNAMPENDA KULIKO KITU CHOCHOTE
Mzazi ni lazima uwe karibu na mtoto kwa kila kitu,tumia
njia zako zote kumuonyesha ni namna gani unampenda,hakikisha unamfanya mtoto
kuwa rafiki,.hii itamfanya mtoto hata unapomgombeza na kumuadhibu ajue unafanya
vile kwa mapenzi ya kumrekebisha na si kumkomoa.
9. USILIMBIKIZE MAKOSA
Mara nyngi wazi tumekuwa na tabia ya kulimbikiza makosa
ya watoto na siku ukiamua kumuadhibu basi unamuadhibu kupitiliza kumbe kafanya
kosa ambalo si hata la kuchapwa lakini wewe unajumlisha mpaka makosa ya mwezi
uliopita unaweza hata kumuumiza ,mzazi hakikisha unamuonya mtoto pale pale
anapofanya kosa lakini sio kumlimbikizia makosa kwanza hii itamfanya mtoto
kuharibika zaidi.
10.
KUCHAPA IWE NI JAMBO LA MWISHO KABISA PALE UNAPOONA NJIA
ZOTE ZIMESHINDIKANA
Wazazi wengine ni wao na kuchapa ,kuchapa na wao,mtoto
akifanya kosa lolote iwe dogo au kubwa yeye ni kuchapa kama sio kuchapwa basi
ni kofi au konzi.Hii si njia sahihi katika malezi,mara nyingi humfanya mtoto
kuishai kuwa sugu na mwishoni kuharibikiwa kabisa,pia humfanya mtoto asiwe na
mapenzi na mzazi,kuwa na nidhamu ya woga na kumfanya mtoto kutojiamini.Nimeshashudia
watoto wengi sana wakipigwa mno,mwishoni hugeuka kuwa watoto watukutu,hakikisha
kupiga inakuwa njia ya mwisho kabisa pale njia zote zinaposhindikana.mada
nayokuja nitaongelea madhara ya kumchapa mtoto kila mara.
Asante sana kwa kutembelea blog hii
Wako mchumi faraja mmasa
Unaweza kutoa maoni yako kwa kucomment hapo chini
Kwa kusoma mada nyingi za malezi bonyeza hii link http://mchumifaraja.blogspot.com/p/wazazi_4.html
0 comments:
Post a Comment