Kulikuwa
na Kijana mmoja alikuwa mwanajeshi alikuwa anabaguliwa jeshini kutokana na
imani yake ya kumwamini MUNGU.Siku moja captain wao akaamua kumdhalilisha mbele
za wanajeshi wenzie
Alimwita
Yule kijana na kumwambia:
We
chukua hii funguo kawashe ile gari pale nenda kaipaki mbele ya jengo la utawala
Yule
kijana akajibu:
-Siwezi
kuendesha gari
Captain
akamjibu:
-Omba
msaada kwa mungu wako unayemwabudu kila siku aje kukusaidia kuendesha gari
tuone
kweli huyo mungu wako yupo.
Yule
kijana akachukua funguo huku akimwomba mungu amsaidie kwenye lile
jaribu,matokeo yake akafanikiwa kuliendesha lile gari na kwenda kulipaki sehemu
aliyoelekezwa kwa usahihi.
Kijana
Yule akatoka nje ya gari na kukuta wanajeshi wenzie wote wanalia,alipowakaribia
wote kwa pamoja na Yule captain wao wakwambia na SISI TUNATAKA TUMWABUDU MUNGU
WAKO UNAYEMTUMIKIA,Yule kijana akashtuka akataka kujua nini kimewapata nao
walikuwa wanamtenga kwa kwa ajili ya mungu aliyekuwa anamtumikia.Captain ndio
alikuwa analia zaidi,akamchukua Yule kijana akampeleka kwenye ile gari
akafungua mbele ya gari akamwonyesha ile gari kumbe walitoa INJINI(ENGINE),lakini
pamoja na kutokuwa na injini gari ilitembea
Yule
kijana akawajibu:
Mmeona?huyu
ndie mungu ninayemwabudu siku zote nimeendesha gari ingawa nilikuwa sijawahi
kuendesha gari hata siku moja lakini
kubwa kuliko yote gari yenyewe pia mlitoa injini ili kumjaribu mungu wangu
lakini gari imetembea.Huyu ndiye mungu anayegeuza yasiyowezekana kuwa
yanawezekana!
Ndugu
msomaji mtumikie mungu kwa roho na kweli daima hatakuja kukuangusha,daima
atajitukuza kwako kwa matendo yake.amen!
Ahsante
kwa kutembelea blog hii
Wako
faraja mmasa a.k.a moa
****daima
kumbuka kutenda mema ,kumbuka duniani tunapita,ishi kwa kumcha mungu kama leo
ndio siku yako ya mwisho duniani lakini tafuta mafanikio kama utaishi
milele!!**********************
0 comments:
Post a Comment