Miongoni mwa vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu ni kupata furaha. Watu wengi wamekuwa na harakati nyingi za kuhakikisha kuwa wanafurahika katika kuishi kwao. Kuna wanaotafuta furaha kupitia kwa rafiki, wapenzi, ndoa zao na hata jamii zao. Ni wazi kwamba kila afanyalo mwanadamu kupitia maamuzi yake, msingi wake huwa ni kutafua furaha, hii haijalishi kama atafanya jambo mbaya au zuri kwa mtazamo wa watu.
Ifahamike, watu wanavuja jasho katika
kufanya kazi kwa sababu wanahitaji mshahara au pato ambalo baadaye hulitumia
katika kufurahi. Wasomi, wafanyabiashara nao wanapohangaka katika hili na lile
ukichunguza utakuta nyuma yao kuna kiu ya furaha.
Hii ina maana kuwa, furaha ndiyo
jambo pekee ambalo watu hulitafuta zaidi. Ni nadra au pengine hakuna mtu ambaye
kwa akili timamu ana kiu ya kupata mabaya na kuhangaika kuyatafuta. Mara nyingi
yakimtokea basi huwa yamejitokeza tu katika safari yake ya kutafuta furaha.
Wezi, majambazi, wazinifu hata watukanaji wote kwa pamoja wanapofanya hivyo
huwa nyuma yao kuna hitaji la kupata furaha.
Pamoja na shabaha ya binadamu kuwa
katika kutafuta furaha, wengi wao wamekuwa hawaipati kwa sababu hawajui njia za
kuipata. Kuna watu wanahangaikia utajiri, wakidhani wakiupata, basi watakuwa na
furaha, lakini baada ya kupata utajiri huo hujikuta hawana furaha. Wengine
huamua kuoa, kuwa na wapenzi na marafiki lakini nao matokeo huwa tofauti na
malengo.
Ingawa kuna matatizo mengi ambayo
yanajitokeza katika maisha ya watu kila siku ambayo huondoa furaha, lakini si
sababu ya moja kwa moja ya kumfanya mtu ahuzunike, eti tu kwa maana kafikwa na
tatizo. Ukichunguza kwa makini utafahamu kuwa furaha si kitu ambacho mtu
anaweza kukipata na kikamtosha. Unaweza kupata kila kitu lakini ukawa huna
furaha.
Ukisema pesa ndiyo furaha, unaweza
kuzipata lakini usifurahike na ukashangaa watu ambao ni masikini wakawa na
furaha tele. Hivyo basi msingi wa furaha ni uelewa wa namna ya kuitafuta na
kuipata. Swali, furaha inapaika wapi na
katika vitu gani? Nibu ni kuishi kwa kuzingatia muongozo ufuatao:
Unaitafutaje furaha?
Watu wengi wanapopata matatizo huwa
hawakubali kuyapokea. Kuna mfano wa mtu mmoja ambaye alikuwa bosi katika
kampuni, siku moja uongozi wa juu uliamua kumshusha cheo kutoka ukurugenzi hadi
mpokea wageni. Bosi huyo alipotelemshwa cheo kwa kiwango hicho hakujiona duni
kwa wafanyakazi wenzake, badala yake alichofikiri yeye ni kwamba watu wote
wanamuunga mkono na kumsikitikia kwa unyama huo wa kushushwa cheo kupitiliza.
Zile fikra za kuhurumiwa na watu
zilimfanya awe na furaha na akawa mtu wa kuwahi kazini kila siku ili watu
wakamuone na kumsikitia, jambo ambalo aliamini kuwa uongozi uliomshusha cheo
ndiyo unaopata aibu mbele ya jamii na wala sio yeye. Kitendo hicho cha kuwahi
kazini na kuonekasna ni mtu mwenye furaha kilimfanya awe mtu wa pekee kwenye
jamii, aliweza kutengeneza maswali mengi kwa watu na hatimaye minong’ono ya kuonewa
ilianza kusikika.
Kilichotokea hatimaye, kampuni moja
kubwa ilipata habari ya kuwepo kwa mtu wa aina hiyo, ikafanya mawasiliano naye
na kumwajiri, bila kujali kashfa zilizokuwa zimemwengua katika wadhifa wake wa
kwanza. Jamaa huyo alipopata ajira mpya alijirekebisha makosa yake ya kugushi
na wizi kwa vile alikuwa amejifunza kilichokuwa kimempata. Bosi huyo aliweza
kuendesha kampuni hiyo kwa mafanikio makubwa, jambo lililowafanya wakuu wake wa
zamani wajute kumuondolea wadhifa.
Hapa tunajifunza kuwa tunapopata
matatizo kinachotufanya tupoteze furaha ni fikra zetu, lakini tukijua kucheza
nazo na kuzielekeza katika mlango wa pili, tunaweza kuyatumia matatizo yetu
kupata furaha pia. Lazima kila mmoja wetu atambue kuwa matatizo ni shule,
tunapoyapata tunajifunza. Lakini hatuwezi kujifunza tukiwa na msongo wa mawazo,
lazima tufanye unafiki fulani wa kimawazo kama alioufanya bosi aliyeshushwa
cheo, yeye hakuangalia wadhifa wake wa zamani, wala namna gani watu wanamtazama
katika kazi yake mpya. Mawazo yanawezaje kutuletea furaha?
Katika hali ya kawaida hakuna mtu
hata mmoja anayeweza kumwambia mwenzake lia naye akafanya hivyo. Kila siku
tunaona na kusikia mengi kutoka kwa
ndugu, rafiki, waalimu wahubiri, wachungaji mapadri wetu na hata kwenye vyombo
ya habari, lakini kusikia huko hakuna maana kuwa ni lazima kutuondolee furaha,
kwani ndani ya akili zetu kuna kitu muhimu ambacho ni maamuzi yetu.
Utawala wa mawazo yetu ni kazi ya
kila siku na uamauzi wa nini ha kufikiri ni suala ambalo lipo kwenye uwezo wa
mwanadamu mwenyewe. Ingekuwa ni lazima kila wazo baya tunaloliona na kulisikia
lazima lituhuzunishe basi tusingekuwa na furaha hata kidogo katika maisha yetu,
kwani hakuna siku ambayo itapita bila kuona, kusikia au kutendewa jambo baya na
mtu mwengine.
Ajali zinatokea kila siku, watu
wanakufa, wanaugua, wanateseka, wanalia, wanaomboleza na kufanyiana hila,
lakini kwa nini hatuyachukulii matukio yote kwa uzito sawa kiasi ha kulia? Ni
kwa sababu tuna uhuru wa kuchagua tulie kwa sababu ya nani na kwa nina? Na hii
ndiyo silaha pekee ya kuyatumia mawazo kutuletea furaha. Yaani kuchagua lipi la
kutuliza na lipi la kutufurahisha na mwisho wa yote tuna uwezo wa kuyatumia
mawazo yetu kuchagua mambo ya kufurahisha na kuyapa kipaumbele, bila kujali ni
mema au mabaya. (Kumbuka mfano wa bosi aliyeshushwa cheo).
Hivyo ni vema wakati tunapokuwa na
mawazo ndani yetu tukazingatia misingi ifuatayo ambayo inaweza kutusaidia kufikia
uamuzi sahihi juu ya kila tunaloona na kulisikia, ili mawazo yasitufanye
tuhuzunike na badala yake tufurahi. Kwanza ni kujipenda wenyewe. Tukijipenda
hatutajihukumu na kujiona duni mbele ya wenzetu na hivyo kutopoteza furaha.
Pili ni kujiamini, kuamini huku kutatuwezesha kuwa na msimamo juu ya maamuzi ya
kila tunachoshibishwa ndani ya mawazo yetu kupitia mawasilia ya sauti na yasiyo
na sauti.
Tatu, kumiliki mawazo yetu
yasichukuliwe na ukubwa au udogo wa tatizo. Udhibiti huu lazima uyaone mambo
yote yanayoingia kichwani kuwa ni ya kawaida kwa vile yapo duniani na
yanawakuta watu kama sehemu ya changamoto za kimaisha. Katika hali ya kawaida
ukubwa au udogo wa tatizo unatokana na mawazo ya mtu husika. Nne, kuwa na
uvumilivu juu ya kila jambo kwa imani kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
Tano na mwisho ni kuhakiki maamuzi yetu kama yako sahihi kabla na baada ya
kutenda jambo.
Kutojiheshimu kunavyohatarisha furaha
yetu?
Ni muhimu kila mtu akaishi kama yeye
alivyo, lakini linapokuja suala la kuchangamana na ulimwengu, lazima kuwe na
kitu cha kujifunza kwa sababu huwezi kuishi nje ya familia na watu wengine.
Kwa msingi huo ili mtu aweze kupata
furaha lazima afahamu namna atakavyoweza kujisahihisha tabia yake kwa
kujiheshimu yeye na kuwaheshimu wengine anaoishi nao. Kwa maana kuishi kama mtu
anatakavyo bila kutazama wengine ni
jambo baya. Hivyo dokezo zifuatazo ni muhimu kwa kila mtu kuzifahamu ili
kuondoa mkwaruzano kati ya mtu na mtu.
A –Wafanyie wengine mema
Furaha haiwezi kuja kama mtu
hajiheshimu mwenyewe na kuwafanyia wengine mema ambayo angependa atendewe. Watu
wengi wamekuwa hodari kutembea na wake za watu, kuiba, kudhuru, kutukana,
kudharau wengine na hata kunyanyasa, bila kugeuza upande wapili wa shilingi na
kufikiri endapo wangefanyiwa wao hali ingekuwaje, si wangepoteza furaha? Sasa
kama jibu ni ndiyo kwa nini wao wawe mahodari kuwaumiza wengine? Ni wazi kwamba
kila mwanadamu angekuwa makini kufanya yale ambayo angependa kufanyiwa, kiwango
ha huzuni kingepungua, na hii ndiyo changamoto kubwa kwa mtu atakaye kupata
furaha lazima awafanyie wengine wema kwanza kabla ya yeye kufanyiwa.
B – Kuwa kiongozi
Katika maisha kuna watu ambao
hawaelewi kuhusu matumizi ya mawazo na namna ya kutenda kama binadamu, hivyo
kwa wale ambao wanaelewa nini maana ya maisha ni vema wakawa viongozi kwa
wengine, viongozi katika kusamehe, kukubali kosa, kutenda haki na kusimamia
ukweli.
C- Kushukuru
Ni watu wachache sana ambao hushukuru
wafanyiwapo mabaya, lakini inashauriliwa kwamba ili kuuita furaha na kupunguza
nguvu ya huzuni ni bora mtu akajifunza kushukuru hata kama amefanyiwa jambo
baya.
D - Kuwa na juhudi
Mambo yote tunayoyafanya lazima
yaambatane na juhudi. Ikiwa tunatafuta majibu ya nini tunataka kifanyeke katika
kupata furaha lazima tuwe na bidii, tusifanye vitu kwa uzembe kwani matokeo
yake ni kushindwa ambako kutatuingiza katika shida ambazo zitatuhuzunisha.
Umeolewa jitahidi kulinda ndoa yako, jitahidi katika kazi na kila jambo ili
usikwame.
E- Kuchunga ulimi
Kuna watu wengi ambao wanapoteza
furaha kwa kutojua namna ya kutumia ndimi zao. Utakuta mtu yuko katika kati ya
watu, anatukana na wakati mwingine kutamka maneno ambayo wenzake hayawapendezi.
Kujiheshimu ni pamoja na kuchuja maneno ya kusema mbele za watu kulingana na
mahitaji yaliyopo, kuropoka ropoka kuna madhara. Kabla hujasema kitu tafakari
kama usemecho kitaleta furaha au huzuni.
Kanuni za kuifikia furaha ya
kweli
Wakati wa kutafuta furaha ya kweli
lazima kujiuliza baadhi ya kanuni za kimaisha kama unazifuata kwa ufasaha,
vinginevyo unaweza kuwa mtafuta furaha lakini usiwe miongoni mwa wanaoipata.
Kama nilivyosema awali kuwa, kuna watu hutafuta furaha kupitia kwa wake/waume
zao, rafiki, wapenzi na hata kwenye mali, lakini mwisho wa siku wanapokuja
kutafakari zaidi hujikuta hawana furaha waliyoitaraji wakati wakihangaikia njia
za kuipata.
Kuna watu ambao mawazo yao yanatamani
sana kupata mtoto na wengine wameapa kabisa kwamba wakifanikiwa kushika
ujauzito watakuwa na furaha, lakini bado kama hawatakuwa makini wao wenyewe watajikuta
wanapata furaha ya muda na hatimaye kutoweka na kuanza kujutia harakati zao,
huku wakianza safari mpya za kufuata furaha kupitia jambo jingine. Hebu
tujiulize maswali haya.
A-Je tunapokuwa tunatafuta furaha
tunatumia uwezo wetu wote au kwa kiwango kidogo? Kama tunatumia kiwango kidogo
basi tujue kuwa hata kama tutapata kitu tunachodhani kitatufurahisha utajikuta
hatufurahi, kwa sababu hatutafanikiwa au tutakuwa na furaha ya muda tu kwa vile
nia yetu hatukuijaza kikamilifu ili tuweze kupata furaha timilifu
B- Je tunafanya sawa katika maamuzi
au tunabahatisha tu?
Endapo tutakuwa tunafanya mambo ya kubahatisha ambayo hatujayahakiki, huzuni yetu itakuwa kwenye makosa na kamwe hatuwezi kufanikiwa kupata yale tunayotaraji yatufurahishe. Kuna watu wanatafuta watoto lakini hawazingatii kalenda za mimba na wengine wanatafuta mali, elimu kubwa, mke mwema, lakini hawako makini katika kufanya maamuzi kwa usahihi. Ni vema tukathibitisha uchaguzi wa mambo ili tufanikiwe kupata yatakayotufurahisha.
Endapo tutakuwa tunafanya mambo ya kubahatisha ambayo hatujayahakiki, huzuni yetu itakuwa kwenye makosa na kamwe hatuwezi kufanikiwa kupata yale tunayotaraji yatufurahishe. Kuna watu wanatafuta watoto lakini hawazingatii kalenda za mimba na wengine wanatafuta mali, elimu kubwa, mke mwema, lakini hawako makini katika kufanya maamuzi kwa usahihi. Ni vema tukathibitisha uchaguzi wa mambo ili tufanikiwe kupata yatakayotufurahisha.
C- Je tunatimiza wajibu wetu au
tunadanganya? Wapo watu ambao walitamani kuoa ili wapate furaha, lakini
walipofanikiwa katika hilo hawakutimiza majukumu yao wakajikuta wanageukwa na
wake/waume zao na kujutia uamuzi wao. Msomaji wangu, unapokuwa katika safari ya
kutafuta furaha kupitia utajiri, elimu, uongozi ni vema ukatimiza wajibu wako,
ili upate matokeo mazuri. Maana kama utakuwa unatamani kufaulu mtihani wako
halafu husomi kwa bidii, sina shaka majibu utakayopata yatakuhuzunisha kwa
sababu lazima ufeli na furaha uliyotaka haitapatikana.
D- Je tunafuata muongozo, au tunakiuka? Kila
jambo tunalotaka kulifanya lina kanuni zake, ukitaka kupika ugali upo muongozo
ambao unakutaka uwe na vifaa, uache maji yachemke na hata kutoharakisha upishi
wenyewe, lengo ni kupata matoke mazuri. Sasa kama tutakuwa kupata furaha ya
kudumu kupitia mambo fulani ni lazima tuyafanye kwa kufuata muongozi na si kwa
kukurupuka. Biashara, elimu, kazi, zote hizi zinamiongozo ambayo lazima
kuifuata kwa matokeo mazuri.
E- Tunatumia tulivyopata au tunavitelekeza?
Wapo watu ambao hutamani kupata kazi, lakini wanapopata hawazitumii, kazi hizo
kwa ukamilifu, badala yake wanakuwa watu wa kufanya ujanja ujanja ujanja kwa
kutoroka na wakati mwingine kutojihusisha na shughuli nyingine kwa lengo lile
lile la kutafuta furaha. Kusema kweli mtu wa namna hii hawezi kuwa na furaha
kwa sababu anayolenga yamfurahishe hayatumii kufurahika na badala yake
anatafuta jambo jingine. Fikiria kuhusu mume, anaoa lakini anaacha kumtumie mke
wake wake anakwenda kwa haw1ara! Hili si jambo jema na kamwe haliwezi kuleta
furaha kupitia mambo tunayoyatafua
kama hujasoma part 1 ya mada hii bonyeza hapa UMEKOSA FURAHA MAISHANI? HIZI NDIZO MBINU ZITAKAZOKUFANYA UREJESHE FURAHA YAKO MAISHANI ,HAIJALISHI UNAPITA KATIKA KIPINDI GANI-PART 1
CREDIT;R.MANYOTA
KARIBU TENA KUITEMBELEA FARAJA MMASA BLOG
WAKO FARAJA MMASA A.K.A MOA
########KUMBUKA KUTENDA MEMA DUNIANI TUNAPITA#####
0 comments:
Post a Comment