Lord
Byron mwanafalsafa na mshairi mahili wa Uingereza aliwahi kuandika maneno haya
“The great art of life is sensation, to feel that weexist even in pain.” Kwa
tafsiri isiyo rasmi ni kwamba Sanaa kubwa ya maisha ni maono, kuhisi mambo ni
madogo hata katika maumivu. Kwangu mimi nimechukulia usemi huo kama somo la
kuwafundisha watu wanaolia kwa matatizo ya aina mbalimbali.
Nafahamu
kwamba katika maisha ya kila siku hayakosekani mambo ya kuumiza. Sina shaka
kuugua, kufiwa, kukosa chakula, kusalitiwa katika mapenzi, kudhurumiwa,
kufilisika na kufutwa kazi ni mambo ambayo huzaa huzuni na machozi miongoni mwa
watu wengi. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba tunalia au kuhuzunika kwa
sababu matatizo yetu ni makubwa au tumekosa kufahamu kanuni ya maisha aliyoitoa
Lord!
Hebu tujiulize ni wangapi tunahuzunikia
mishahara midogo tunayolipwa makazini mwetu? Je katika huzuni hizo tulishawahi
kuwaza kwamba kuna binadamu wengine hawana kazi na wanahangaika kutafuta
shilingi mia tano kwa kuuza mihogo na karanga kwenye kona za mitaa huku wakiwa
juani?. Kama hao wapo ukubwa wa tatizo la kukosa kazi unaotuliza kila siku uko
wapi?
Uko wapi ukubwa wa tatizo la kutokuzaa wakati
kuna waliozaa na watoto wote wakafa. Kimsingi uwiano wa shida na uhimili wake
unaopatikana baina ya mtu na mtu, kamwe sifa ya huzuni hailetwi na ukubwa wa
tatizo, isipokuwa ni kukosekana kwa sanaa ya kuishi, yenye maono na hisia za
kupunguza mambo makubwa kuwa madogo.
Katika hisia, mwanadamu hawezi kuzuia machozi
ya furaha au huzuni yasitoke, maana nilisoma katika Biblia kuwa hata Yesu
alilia pale alipopata habari kwamba rafiki yake Lazaro amekufa. Lakini pamoja
na kilio hicho hakusita kuita maono na kuona kwamba tatizo lililokuwa mbele
yake lilikuwa dogo, akaamua kuchukua hatua ya kuwaagiza wanakijijini waliondoe
jiwe na yeye kutajwa kumfufua kwa kutumia uwezo wake (Haya ni ya kidini
siyajadili sana katika mada hii).
Ifahamike kwamba kila mwanadamu ana uwezo wake
wa kufanya, zaidi ya tatizo analokutana nalo, lakini uwezo huo hauji kama sanaa
ya maono na ‘udogoshaji’ matatizo haujapewa kipaumbele. Kuna watu wanalia kila
siku kwa kuhitaji utajiri, lakini hawafikii malengo kwa sababu wanaona
umasikini ni jambo kubwa na kuufikia utajiri ni jambo kubwa pia.
Kwa mujibu wa utafiti wa William Frey mkemia
na Mkurugenzi wa Kituo cha Dry Eye and Tear Reseach cha Minneapolis, watu hulia
katika makundi matano tofauti ambayo ni: Wenye kujawa na huzuni zinazosababishwa na matatizo ya kimaisha 49%.
Wanaolia
kwa furaha ni alisilimia 21, hasira 10% na huruma 7%, huku wenye wasiwasi
wakilia kwa kiwango cha asilimi 5 juu ya wenye hofu wanaolia kwa asilimia 4.
Lakini,
pamoja na kuwepo kwa makundi hayo sita, mwanadamu mwenyewe anatajwa kuwa na
uwezo wa kuyabadili maono yake kwa kila kundi na kupata matokeo tofauti kabisa,
kwani hasira ikipunguzwa kwa kuona kichocheo kilichojaza hasira ni kidogo pumzi
hushuka na mtu hujiona mwenye utulivu tofauti na mwanzo.
Vivyo
hivyo, kwa anayelia kwa huzuni, huruma, wasiwasi na hofu! Kwa mantiki ile ile
hakuna haja ya kuhuzunika kwa kiwango cha juu, wakati kuna kiwango cha chini
cha kujiweka huru, nacho ni cha kutazama mambo makubwa kama madogo yasiyodumu
na kwamba saa, siku, miaka michache
ijayo yatapita. Jiulize hapo ulipo msomaji wangu ni kitu gani
kinakuliza? Fahamu kwamba hulii au kuhuzunika kwa sababu matatizo ni makubwa,
bali umekosa ufahamu wa maono.
Hebu
chukua jukumu la kudharau shida zako kwa kujilinganisha na wengine ambao bila
shaka wanakuzidi matatizo. Fanya hivyo kila unapokabiliwa na tatizo, usilione
tatizo ni kubwa kwa takwimu, lichukulie kuwa ni dogo kisha uanze
kulishughulikia, utaona linamalizika kwa ushindi mkubwa. Kamwe usijaribu kulitatua
ndani ya maono yanayolikuza, hutapata matokeo mazuri.
Ukiwa
ni umasikini uone ni mdogo, kututokuzaa, kukosa kazi, kuteswa na mume na
matatizo yote yatakayokukuta katika maisha yako yaone ni madogo kisha tumia
nguvu zako zote kuyakabili nina hakika utayashinda kirahisi.
Lord Byron aliguindua kanuni aliyoipa jina la
Byronic Hero, ambayo ilikuwa na misingi ya kuishi kwa maono na kupunguza ukubwa wa mambo kwa kutumia fikra.
Wengi walipata mafanikio ya kutisha. Jaribu kupunguza matatizo, badala ya kuyakuza
kwa kuona hayawezekani kutatuliwa, utaona maajabu. Tambua kuwa tatizo lako si
kubwa bali unalikuza katika mawazo yako, kwa kuwa wapo wenye matatizo makubwa
zaidi yao na hawalii kama wewe.
kwa ushauri zaidi unaweza piga namba 0658494977
kwa ushauri zaidi unaweza piga namba 0658494977
Ahsante
kwa kutembelea blog hii
Wako
Faraja mmasa -moa
Credit bro R.manyotaFaraja mmasa -moa
0 comments:
Post a Comment