Vifaranga wanapotunzwa vizuri kama hawa hukua vizuri na kuwa
kuku wenye afya
Kwa karne na miaka mingi, ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu
na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana,
ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara.
Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa
wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia
siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa
ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.
Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula
tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya
kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili
vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa:
• Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye
joto kwa wastani unaohitajika.Kuku wenye afya 1
• Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na
isiyokuwa na vimelea.
• Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks)
siku ya kwanza.
• Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa
kideri.
• Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa
wa gumboro.
• Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.
• Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro
• Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata
chanjo ya ndui.
Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku
wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na
mazao bora, na hatimaye kupata faida.
Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii
itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.
**Kamwe usiwape kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza
kusababisha madhara makubwa kwa kuku na kusababishia hasara***
SOURCE MKULIMA MBUNIFU
0 comments:
Post a Comment