WATAFITIi wa nchini Israel walibaini kuwa, mtu
anayekunywa chai mara kwa mara ana uwezo wa kuishi muda mrefu tofauti na yule
asiyependa chai
Aghalabu maisha ya mwanadamu yeyote yule yapo
mikononi mwa muumba wake, ambaye hujua lini muda wa kuishi wa kiumbe wake
utakwisha. Lakini mtindo wa maisha yetu usiojali kanuni za afya, umeonyesha
kuwa ndicho chanzo cha watu wengi kuishi maisha mafupi.
Kiwango cha maisha ya binadamu sasa
kinapunguzwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, mtindo wa maisha na
mazingira, lakini wanasayansi na wataalamu wa afya wamekuja na mbinu ambazo
zinatajwa kusaidia kuongeza miaka yako ya kuishi.
KUNYWA CHAI
Watafiti wa nchini Israel walibaini kuwa, mtu
anayekunywa chai mara kwa mara ana uwezo wa kuishi muda mrefu tofauti na yule
asiyependa chai.
Chai, hasa ya kijani (green tea) ina ondoa
sumu iitwayo ‘polyphenols’ ambayo husaidia mwili wako kupambana na magonjwa ya
moyo. Wataalamu hao wanasema, chai iliyochemka vizuri au pakiti ya majani ya
chai kukorogwa vyema katika majimoto, yafaa zaidi. Kwa kifupi, chai ikolee
majani.
KUSIMAMA KWA
MGUU MMOJA KILA ASUBUHI
Inaweza
kuonekana kuwa ni jambo la ajabu, lakini wanasayansi wamebaini kuwa kusimama
kwa mguu mmoja asubuhi kunasaidia kuimarisha misuli ya mgongo, nyonga na tumbo
na kuupa uwiano uti wa mgongo.
Mtaalamu wa viungo anasema, zoezi hili jepesi
likifanywa kila siku, linatoa manufaa ya muda mrefu na linakukinga kuvunjika
mifupa kwa urahisi hasa unapoanza kuzeeka. Tafuta marafiki sita unaowaamini
Kuwa na marafiki wazuri na familia ambayo unaiamini ni siri moja kubwa ya
kuishi miaka 100.
Utafiti uliofanywa na kitengo cha Maisha na
Mazingira katika Chuo Kikuu cha Australia, ulionyesha kuwa kupata watu wa
kukupa msaada na kukufariji wakati wa huzuni kunasaidia kuongeza umri wa kuishi
kwa kuzalisha kemikali ya ‘furaha’ inayofahamika kama dopamine na oxtocyin
ambavyo huusaidia ubongo.
Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma,
anasema unapokuwa na tatizo, kisha ukalihifadhi moyoni, unaunda uchungu ambao
unakuathiri. Anasema, mwili wa mtu unaathiriwa kutokana na tabia au matendo ya
moyoni, unapohifadhi tatizo bila kupata ushauri unakuza tatizo hilo.
“Marafiki au hata ndugu wa kumweleza tatizo
lako ni muhimu, wanaweza kukupoza,” anasema
USISHIBE
SANA
Wakazi wa kisiwa cha Okinawa, nchini Japan,
wanaongoza kwa kuwa na kiasi kidogo cha watu wenye unene uliopitiliza (obesity)
na wanasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi zaidi ya miaka 100.
Siri yao kubwa ni kuwa hawali wakashiba kwa zaidi ya asilimia 80.
Watafiti wa Marekani pia, wamebaini kuwa,
binadamu wanaweza kuishi miaka mingi zaidi iwapo chakula wanachokula
kinapunguzwa kwa robo tatu. Ina maana kwamba kula kidogo kunaufanya mwili wako
usiwe na kazi kubwa ya kumeng’enya, hivyo kuupa nafasi ya kuwajibika na kazi
nyingine.
Mtaalamu wa chakula na lishe, anasema, mtu
hatakiwi kula akashiba bali anatakiwa aache njaa kwa mbali ili kutoa nafasi ya
maji na mmengenyo kuchukua nafasi.
LALA KWA
MUDA MREFU
Ukosefu wa usingizi unakuweka katika hatari
kubwa ya kupata maradhi ya msongo wa mawazo na moyo. Kupata makunyanzi na mwili
kuchoka.
Mabadiliko kidogo tu ya kitabia yanaweza
kuleta mapinduzi makubwa katika afya yako. Wanaopata usingizi wa kutosha si
rahisi kupatwa na kiharusi au shinikizo la damu.
PIGA MSWAKI
Maradhi ya fizi, ni maradhi yaliyopata
umaarufu duniani. Dk James Russel wa kituo cha tiba cha Hope, anasema, meno na
fizi ni chanzo cha magonjwa mengi ambayo wengi hudhani hayahusiani na afya ya
kinywa. Maradhi ya fizi yanatajwa kuwa chanzo cha saratani za aina fulani,
maradhi ya moyo, ubongo na hata kisukari.
KUWA MAKINI
Utafiti uliofanywa na Mwanasaikolojia wa
nchini Marekani, Dk Howard Friedman unasema kuwa, umakini wa mtu ni kigezo cha
urefu wa maisha yake. Watu ambao wapo makini na maamuzi, matumizi ya fedha na
ambao wanapenda kuweka kila kitu sawa na kufanya mambo yao kwa uangalifu,
wanaweza kuishi kwa muda mrefu.
KWA NINI? Dk Kitila Mkumbo, Mwanasaikolojia wa
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) anasema, unapokuwa makini unafanya uamuzi
mzuri ambayo hupunguza kiwango cha kuishi maisha hatarishi.
“Umakini unamsaidia mtu kuepuka tabia
hatarishi kwa mfano ngono zembe, kuvuta sigara, mambo ambayo yanahatarisha
afya,” anasema.
Anasema, mtu anayepangilia mambo yake na kuwa
makini kwa mfano kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa kunakuepusha na
maambukizi ya maradhi mbalimbali.
USIWEKE
MATUNDA KWENYE JOKOFU
Unaweza
kufikiri kuwa, kuyaweka matunda katika jokofu, unayafanya yadumu kwa muda
mrefu, lakini tafiti zinaonyesha kuwa, matunda yaliyopoozwa kwa baridi ya
jokofu, yanapungukiwa vitamini muhimu kuliko matunda yanayowekwa katika hali ya
kawaida.
Kwa mfano, nyanya na pilili ni vyema kuwekwa
katika bakuli kuliko katika jokofu. Matunda mengi yanasaidia kuondoa sumu
mwilini hivyo lishe zake zikibaki bila kuharibiwa, husaidia kujenga moyo imara
na kupunguza kiwango aina fulani za saratani.
KUFANYA
TENDO LA NDOA ANGALAU MARA MBILI KWA WIKI
Utafiti mkubwa na uliothibitishwa wa Welsh na
wenzake wa Hospitali ya Royal Edinburgh, Uingereza ulibaini kuwa wale
wanaofanya mapenzi mara moja kwa mwezi wapo katika hatari ya kufa mapema,
ukilinganisha na wale wanaofanya mapenzi mara mbili kwa wiki.
Welsh anasema, tendo la ndoa linapunguza
msongo wa mawazo na kumfanya mtu apate usingizi mzuri. Msongo wa mawazo
unasababisha maradhi ya moyo na kisukari. Dk Mkumbo anasema, tendo la ndoa ni
jambo la afya na husaidia katika kupunguza msongo wa mawazo na kuupa mwili
uchangamfu. Hata hivyo Dk Mkumbo anasema hajawahi kusikia idadi ya siku za
kufanya mapenzi kama ni mara moja au mbili kwa wiki, bali anaamini kitendo
chenyewe kina umuhimu wake kiafya.
Kwa nini Wajapan wanaishi maisha marefu?
Inaelezwa kuwa Wajapan ni taifa linaloongoza kwa kuwa na watu wanaoishi muda
mrefu kuliko mataifa mengine. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaeleza
kuwa, raia wa Japan wanaishi maisha marefu zaidi. Kwa mfano, mwanaume mzee
kuliko wote aliyevunja rekodi ni Jiroemon Kimura, kutoka Kyotango, Kyotto,
Japan aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116. Siri yao kubwa ni kula
chakula chenye afya ikiwemo samaki badala ya nyama nyekundu.
Hawanywi maziwa, au bidhaa zozote za ng’ombe.
Nafaka jamii ya soya ambazo zinasaidia kuondoa maradhi ya moyo. Wanakunywa chai
kwa wingi, hasa ya kijani, wanakula kiasi kidogo cha chakula, hawatumii magari
mara kwa mara na wanatumia vyoo vya kuchuchumaa badala ya vya kukaa
SOURCE JAMII FORUMS
KARIBU TENA FARAJA MMASA BLOG
X+3P
*SELF FULFILLING PROPHECY*
0 comments:
Post a Comment