Habari ndugu wasomaji wa BLOG hii, samahani kwa kutokuwa hewani muda mrefu, nafahamu blog hii inawasaidia watu wengi mno katika mambo mambo mbalimbali, pamoja na kutokuandika kitu chochote kwa zaidi ya miaka MITANO (5) sasa lakini katika muda wote huo nimeendelea kupokea simu na msg mbalimbali za watu kuomba ushauri katika mambo mbalimbali. Nilikuwa nimebanwa na majukumu mengine lakini kuanzia muda sio mrefu baada ya maboresho tunayoyafanya kuibadilisha BLOG hii na kuwa WEBSITE tutaanza tena kupost mada mbalimbali ambayo imani yetu zitawasaidia kwa namna moja au nyingine katika kukabaliana na maisha yetu ya kila siku. Wasomaji wangu mmenishtua baada ya baadhi ya post kukuta zimesomwa na watu zaidi ya 10,000. WEBSITE pia tutaibadilisha JINA tutawafahamisha hapa.Ahsanteni sana sana
Sunday, August 23, 2020
Monday, April 27, 2015
KABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA,USIKATE TAMAA
KUNA wakati maisha yako yanaporomoka kutokana na kupatwa na misukosuko ya maisha kama vile kufiwa na mke, mume au mtoto wako, kusalitiwa na marafiki uliowategemea maishani mwako, kukimbiwa na mke au mume wako, kufilisika, kupoteza kazi uliyokuwa ukiitegemea, au daktari kukuambia kuwa ugonjwa unaokusumbua si rahisi kupona.
Hali hiyo inapokutokea, unajikuta unakata tamaa ya maisha na kujiona kuwa hustahili kuishi katika dunia hii inayokuzunguka, lakini kumbuka hiyo ni njia ya kupitia katika maisha haya tunayoishi. Hivyo ni vizuri kumtafuta rafiki yako wa karibu au kiongozi wako wa dini kwa msaada zaidi. Kwani viongozi wa dini mara nyingi wamekuwa washauri wazuri katika maisha yetu ya kila siku.
Pia ukubaliane na hali ile ambayo huwezi kuibadilisha katika maisha yako. Na kukataa kuendekeza nafsi yako katika hali ya kujisikitikia kwani hali ya kujihurumia ni ugonjwa, kama vile acid. Hali hiyo itakuondolea hadhi yako, itakuongezea sononeko na kukata tamaa. Itakuharibia uhusiano wako na wengine. Itakusababishia hali ya kuwa na chuki. Hakuna jambo zuri litakalokujia katika maisha yako kutokana na hali hiyo ya kujisikitikia.
Usichukue maumivu yako kwa wengine. Unaporuhusu maumivu huumizi watu wengine bali unajiumiza wewe mwenyewe. Iambie nafsi yako kuwa unahusika na vitendo au tabia zako mwenyewe. Hakuna atakayeiumiza nafsi yako ila wewe mwenyewe. Usifanye ukaidi. Kubaliana na ukweli. Si wakati wote maisha yanakuwa sawa na ya kuridhisha. Haijalishi hali inayokutokea katika maisha yako, hali ya kukata tamaa, ndoto zako hazikutimia bado kuna tumaini katika maisha yako.
Saturday, March 28, 2015
Kiri Kosa, Jifunze, Jipe Nafasi Ya Kuanza Upya.
Katika
safari ya maisha, ni jambo la kawaida kabisa kukutana na vikwazo vinavyoweza
kukatisha tamaa. Ukubwa wa vikwazo au changamoto hizo, zinaweza kukusababishia
ukaiona dunia kama imegeuka, au wakati mwingine ukatamani ipasuke uingie ndani
yake.
Yapo mambo
mengi yanayoweza kukufanya ufikirie hivyo. Huenda yakawa ni makosa ya
kibinadamu, matatizo, changamoto, kukatishwa tamaa na baadhi ya watu au
kujiponza mwenyewe kutokana na hili au lile. Lakini ukikaa chini, ukatafakari
utatambua kuwa hakuna binadamu asiyeteleza kwa kufanya makosa au kupitia
changamoto kwenye safari ya maisha.
Hivyo wakati
mwingine unapaswa kuelewa kuwa kwa kila linalokupata, bado unayo nafasi ya
kufungua ukurasa mpya. Kupatwa na mitihani katika maisha, mara nyingi ni darasa
mojawapo tunalotakiwa kuliangalia kwa umakini ili kupata somo au fundisho
lililo ndani yake.
Ikiwa
mtihani huo umekuja kutokana na kosa ulilofanya, ni vyema kukubali kama
umekosea na kisha kujipa nafasi ya kusonga mbele. Tunaelewa kuwa maisha ya kila
mmoja wetu kwa namna moja au nyingine yanaendeshwa na misimamo mbalimbali. Kuna
wale wanaoamini kuwa wao hawawezi kufanya
jambo Fulani na wakati mwingine kuamini kuwa hawawezi kukosea kabisa.
Thursday, October 16, 2014
hi!
Nimewamisi sana,very soon nitaanza kuandika tena makala mbalimbali,muda umekuwa ni kikwazo kikubwa.Mbarikiwe wapendwa,mungu awabariki katika kila mfanyanyo na mpangacho .
Ahsanteni kwa kuendelea kusoma Blog hii.
Wednesday, May 7, 2014
NAMNA YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA
Mpango wa biashara unasaida kufanya
uamuzi mbalimbali kusuhusu mwenendo mzima wa biashara, kupima mwelekeo na
ukuaji wa biashara.
Mchanganuo wa biashara ni andiko
linalofafanua namna biashara inavyoweza kuanzishwa au kuendelezwa. Kitaalam,
unatakiwa uwe na mpango wa biashara kabla ya kuanza biashara yoyote.
Mpango wa biashara unasaida kufanya
uamuzi mbalimbali kusuhusu mwenendo mzima wa biashara, kupima mwelekeo na
ukuaji wa biashara.
Pia mwenendo wa biashara
unasadia ugundua mapungufu katika
uendeshaji biashara na kubaini fursa za kupanua biashara. Ufuatayo ni mtririko
wa mchanganuo wa biashara.
Jalada la nje: Linahusisha jina la
biashara, muda wa mpango (mfano. 2013 – 2015), anuani ya biashara, toleo, jina
la aliyeandaa, mwaka pamoja na kuonyesha mchanganuo unaelekezwa kwa nani.
DIBAJI
Sehemu hii huandikwa muhtasri wa
mambo mbalimbali yaliyoanishwa katika mchanganuo mathalani, aina ya biashara,
bidhaa au huduma zinazotolewa kwa ufupi, mpango wa mauzo, mpango wa ukuaji kwa
mwaka, soko lengwa, mtaji unaohitajika, namna mwekezaji au mdau anavyoweza
kunufaika iwapo akiwekeza au benki ikikupatia mkopo namna gani utalipa.
24 Things To Always Remember
Your
presence is a present to the world.
You
are unique and one of a kind.
Your
life can be what you want it to be.
Take
the days just one at a time.
Count
your blessings, not your troubles.
You
will make it through whatever comes along.
Within
you are so many answers.
Understand,
have courage, be strong.
Friday, May 2, 2014
JINSI YA KUISHI NA WATU
Wako Faraja Mmasa
Thursday, May 1, 2014
MBINU ZA KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA YAKO.
Karibu katika blog hii ,natumaini u mzima wa afya njema maana
mungu wetu anaendelea kutupigania.Leo
nilitaka kuongelea mada hii ya kuongeza mauzo katika biashara,kama tunavyojua
moyo wa biashara ni mauzo,kama hakuna mauzo basi hakuna biashara.Kabla sijaanza
kulielezea zaidi mada hii kama ndio mara yako ya kwanza kusoma blog hii,basi
pia mwenye blog hii pia ni mshauri katika mambo ya biashara ,pia katika maswala
ya saikolojia na Afya ,kama unatatizo lolote basi unaweza kupiga simu au kutuma
msg katika namba 0658494977 kwa ushauri zaidi.
Kama nilivyosema hapo mwanzo Mauzo ndio moyo wa biashara,kama
hakuna mauzo hakuna biashara,kama ilivyo kwa mwanadamu bila Moyo hakuna Uhai
,hivyo hivyo kwenye biashara kama hakuna Mauzo basi hakuna Biashara,basi ni
lazima kwa mfanyabiashara yoyote yule mara zote kusumbua akili yake namna gani
anaweza kuongeza mauzo katika biashara yake,leo nitaongelea mambo ya msingi matatu
katika kukuza mauzo katika biashara yako
MBINU ZA KUPUNGUA UZITO
Inaonekana
kuwa watu wengi hatujui ni kiasi gani cha kalori za chakula tunachotakiwa kula
kwa siku. Kuna umuhimu mkubwa kufahamu kuwa, tunatakiwa kula kiasi cha kalori
sawa na kalori zinazotumiwa na miili yetu ili kudhibiti uzito na kujiepusha na
unene.
Hata
hivyo kuna mambo mengi yanayoathiri kiwango cha kalori kinachotakiwa kuliwa kwa
siku kama vile jinsia, umri, uzito, urefu na aina ya kazi na shughuli za mwili.
Lakini kabla hujaanza kusoma mada hii,kama umejaribu mara nyingi kupungua uzito
imeshindikana au hupati matokeo unayotaka basi piga namba 0658494977 kwa ushauri na kupewa njia sahihi ya
kupunguza uzito ambayo utaanza kuona matokeo ndani ya wiki moja
Monday, April 28, 2014
NJIA YA KUWEKA AKIBA NA KUONGEZA MTAJI KATIKA BIASHARA YAKO
Moja ya nguzo za mafanikio ya wajasiriamali ni
elimu, ikwemo ya kuwaongezea upeo wa kutafuta mitaji.
Ni ijumaa nyingine tunapokutana tena katika
kona hii ya mjasiriamali, hii ni kona ambayo maudhui yake ni kuona namna bora
ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kuanzisha na baadae kuendeleza
biashara zao na kupata mafanikio wanayotamani.
Makala iliyopita ilijadili juu ya umuhimu wa
kuweka akiba ili kujikinga na majanga.
Kuna msemo unasema akiba haiozi, mjasirimali
unapaswa wakati wote kukumbuka msemo huu ili uwe chachu ya wewe kujiwekea akiba
kwa malengo mbalimbali.
Ukiwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kutokana
na mapato yako unayoyapata utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kukabilina na
majanga mbalimbali ambayo yanaweza kutokea katika biashara yako, kumbuka una
nafasi ya kubadilika na kujipanga upya.
Leo katika kona ya mjasiriamali tutakumbushana
juu ya baadhi ya njia ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kuweza
kuongeza mitaji ya biashara zao. Katika njia mbalimbali za kuongeza mitaji zipo
zinazoweza kusaidia na nyingine kuumiza.
Mitaji ya biashara ni kilio cha wengi aidha
kwa wale walio katika ujasiriamali au kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye
ujasiriamali. Wengi hulia kwamba watapata wapi mtaji kwaajili ya kuanzisha
biashara au kwaajili ya kuendeleza biashara.
Wajasiriamali wanapaswa waelewe kwamba kuna
njia mbalimbali za kuweza kuongeza mtaji katika biashara wanazofanya. Muhimu
zaidi ni kufahamu njia hizi ili kuweza kuangali ni ipi kwa hatua uliyofikia
inaweza kukusaidia zaidi badala ya kukuumiza.
Yafaa pia kujiuliza je ni sababu zipi
zinazopelekea wewe kuwa na hitaji la ongezeko la mtaji katika biashara
yako na nini matokeo tarajiwa. Kujiuliza
maswali haya na mengine itakusaidi kufanya uamuzi sahii. Zifuatazo ni njia za
kuongeza mitaji ya biashara yako.
Njia ya kwanza ni uwekaji wa akiba. Uwekaji wa
akiba ni njia ya kwanza ambayo inaweza kukusaidia katika kukuza mtaji wako wa
biashara. Kma utakuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ni rahisi kwako kutumia
akiba ili uweze kukuza mtaji wako.
Iwe kwa mjasiriamali mwenye biashara mpya au
inayoendelea ni muhimu sana kufikiria kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji
wa biashara. Uwekaji wa akiba ni moja ya njia ya kukuza mtaji ambayo haina gharama wala matatizo
kuliko nyingine yoyote.
Uwekaji wa akiba ni njia inayoonekana ngumu
kati ya watu kwasababu ni njia ambayo inahitaji nidhamu ya hali ya juu.
Unapotaka kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara au kuendeleza
biashara unahitaji nidhamu katika matumizi ya fedha zako.
Jiulize je matumizi ya fedha zako yakoje? Ni
yapi yamekuwa matumizi ya msingi na yapi si ya msingi, kwanini usipunguze au
kuacha matumizi yasio ya msingi na kuweka akiba ili kuweza kukuza mtaji
kwaajili ya biashara yako.
Jiulize unatumia kiasi gani cha fedha zako
kwaajili ya ‘vocha’, unatumia kiasi gani kwaajili ya pombe, unatumia kiasi gani
kwaajili ya starehe, vipi michango ya harusi, je unatumia kiasi gani kwaajili
ya burudani nyingine ambazo si za msingi!
Kaa chini na utafakari juu ya mapato na
matumizi yako na angalia ni kwa namna gani unaweza kuweka sehemu ya mapato yako
kama akiba kwaajili ya aidha kukuza mtaji wa biashara unayofanya au kuanzisha
biashara mpya na malengo mengine ya baadae.
MAMBO KUMI YA MSINGI YA KUFUATILIA UNAPOKUWA UNAJIANDAA NA MITIHANI
Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii
ya Faraja Mmasa Blog, natuamini ni mzima wa afya njema maana mungu wetu mpendwa
anatupigania kila sekunde.Asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mara kwa mara wa blog
hii lakini pia nikupongeze kwa kuwa mfuatiaji wa mara kwa mara kwa kuwa kila
unapoingia katika blog hii basi kuna kitu kipya unajifunza kila siku
katikachokusaidia katika maisha yako ya
kila siku.Mada ninayotaka
kuilezea leo inahusu hasa wanafunzi wa kidato cha sita wanaokwenda kujiandaa na
mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita,Mimi ninawaombea sana kwa mwenyezi
mungu kila mmoja akafanye mitihani kwa utulivu na kuweza kusonga mbele, nimeinadika
mada hii kwa ajili ya wanafunzi wote wa kidato cha sita lakini pia na mimi pia
mdogo wangu kipenzi wa mwisho Jackline Kaboko anajiandaa kufanya mtihani
huo,kwa hio nikaona sio vyema kukaa na kumuelezea nini cha kufanya peke yake
basi ,bali niongee na wanafunzi wote wanaojiandaa na mtihani huu.Mada hii pia
nitaifundisha katika Redio ya Sibuka 94.5 fm siku ya jumatatu na alhamisi
kuanzia saa tisa na dakika 20,hivyo basi
pia unaweza kunisikiliza kupitia Radio.
Friday, April 25, 2014
NI MUHIMU KUZINGATIA UTUNZAJI WA VIFARANGA
Vifaranga wanapotunzwa vizuri kama hawa hukua vizuri na kuwa
kuku wenye afya
Kwa karne na miaka mingi, ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu
na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana,
ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara.
Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa
wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia
siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa
ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.
Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula
tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya
kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili
vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa:
• Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye
joto kwa wastani unaohitajika.Kuku wenye afya 1
• Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na
isiyokuwa na vimelea.
• Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks)
siku ya kwanza.
• Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa
kideri.
• Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa
wa gumboro.
• Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.
• Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro
• Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata
chanjo ya ndui.
Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku
wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na
mazao bora, na hatimaye kupata faida.
Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii
itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.
**Kamwe usiwape kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza
kusababisha madhara makubwa kwa kuku na kusababishia hasara***
SOURCE MKULIMA MBUNIFU